10 Aprili 2021 - 16:22
Qais al Khazali: Saudia na Imarati hazijafanya kitu kingine ghairi ya uharibifu nchini Iraq

Katibu Mkuu wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ya nchini Iraq amekosoa hatua za Marekani, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) dhidi ya nchi hiyo na kusisitiza kuwa Wairaqi hawana hata chembe ya imani na nchi hizo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Qais al Khazali amesisitiza kuwa, iwapo Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zina azma ya kweli ya kuanzisha uhusiano mpya na Iraq zinapasa kuomba radhi kwa kitendo chao cha kufadhili ugaidi na kumwaga damu wa wananchi wa Iraq. 

Al Khazali amesisitiza kuwa, Iraq haijashuhudia chochote kutoka kwa Saudi Arabia na Imarati ghairi ya ushari na uharibifu na kwamba nchi yoyote ambako Imarati na Saudi Arabia inakotia mguu huwa haina mustakbali mwingine isipokuwa maangamizi, mauaji na vita vya ndani. 

Katibu Mkuu wa wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ya nchini Iraq ameongeza kuwa: "Hatuwezi kuziamini kirahisi Riyadh na Abu Dhabi, tumepoteza mashahidi wengi kupitia harakati za uharibifu za nchi hizo. Saudi Arabia pekee ilituma magaidi elfu tano wa kujilipua kwa mabomu ambao walijiripua baina ya wananchi wa Iraq." 

Kiongozi huyo wa Iraq ameashiria pia uwepo kinyume cha sheria nchini Iraq wanajeshi magaidi wa Marekani na kusema, wanajeshi hao ambao hawahitajiki wanapasa kuondoka nchini Iraq katika muda ulioainishwa. 

342/