12 Juni 2025 - 23:59
Tafsiri ya Surat Al_Baqarah, Aya ya 200-202 | Mushrikina walirithi Ibada ya Hijja kutoka kwa Nabii Ibrahim(as) lakini walitia uzushi mwingi ndani yake

Wanaotaka Starehe za Dunia, humuabudu Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Dunia. Hao ndio wale wasiokuwa na lolote katika Akhera.

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Pamoja na kuwa Mushirikina walirithi ibada ya Hijja kutoka kwa Nabii Ibrahim (a.s) lakini walizua mambo mengi sana yakiwemo kutajawa wakale wao kwa fahari; ndipo Mwenyezi Mungu akawaamuru kuliacha hilo, baada yake wamtaje Mwenyezi Mungu na jinsi alivyowaneemesha.

Kwa vile Yeye ndiye aliyewaneemesha wao na hao mababa zao.

201 - 202 Na Katika ibada nyingi, ikiwemo Hijjah, huwa kuna aina mbili za watu: Kwanza ni wale wanaotaka starehe ya dunia tu, wanamwabudu Mwenyezi Mungu kwa ajili ya dunia. Hawa ndio wasiokuwa na lolote akhera. Pili, ni wale wanaofanya kwa ajili ya dunia yao na akhera yao. Hawa ndio walioridhiwa na Mwenyezi Mungu na kesho watalipwa mema.

Mwenyezi mungu atujaalie tuwe ni kundi hili la pili, ibada zetu ziwe na manufaa ya Dunia na Akhera, InshaAllah.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha