Main Title

source : parstoday
Jumatano

9 Juni 2021

18:42:48
1148975

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa azabwa kibao + Video

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amezabwa kibao wakati akiwa ziarani kusini mashariki mwa nchi hiyo. Katika kuonesha kuwa bado watu wanampenda, rais huyo anayeshindwa kuficha chuki zake dhidi ya Uislamu, alikwenda haraka kuwapa mikono watu waliokuwa wamesimama pembeni. Mtu wa kwanza kumpa mkono ametumia fursa hiyo hiyo kumzaba kibao.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Habari hiyo imeenea kwa kasi kubwa kuliko umeme katika mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari kama shirika la habari la Sputnik, BFM TV na RMC Radio.

Tukio hilo lilitokea jana Jumanne wakati rais huyo wa Ufaransa alipokuwa anatembelea mji wa Drôme wa kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika la habari la Sputnik limesema kuwa, watu waliokasirishwa na siasa mbovu za Macron wamemsusia rais huyo wa Ufaransa na hata hao waliokwenda kumlaki inaonekana walikwenda kwa ajili ya kudhihirisha hasira zao kwake kwani mara baada ya kutoa mkono, mtu huyo aliyekuwa amevaa barakoa amemzaba kibao kikali Macron.

Walinzi wa rais huyo wa Ufaransa wameingilia kati karaka na kumuangusha chini mtu huyo, huku watu wengine waliokuwepo hapo wakisikika wakimcheka Macron.

Taarifa hiyo imesema kuwa, kabla ya kupata fursa ya kumzaba kibao rais huyo wa Ufaransa, mtu huyo alikuwa amesikika akisema: "Mauti kwa Macron!" Vyombo vya habari vya ndani ya Ufaransa vimetangaza kuwa watu wawili wametiwa mbaroni kwenye tukio hilo.

Emmanuel Macron, rais wa Ufaransa aliyezabwa kibao, amepoteza mno umaarufu wake kiasi kwamba katika kipindi cha miaka mwili iliyopita, umaarufu wake umepungua kutoka asilimia 48 hadi 38.

Ikumbukwe kuwa, Macron amekuwa akitangaza waziwazi kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu ikiwa ni pamoja na uchoraji wa vikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW. Ni kama vile aibu ameanza kuipata hapa hapa duniani rais huyo wa Ufaransa.

342/