Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

23 Julai 2021

10:23:44
1162527

Kiongozi Muadhamu apokea dozi ya pili ya chanjo ya Corona iliyozalishwa Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amepigwa dozi ya pili ya chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Covid-19 ambayo imetengenezwa na wataalamu wa ndani ya nchi ya COVIran Barekat.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taarifa ya Ofisi ya Ayatullah Ali Khamenei imesema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepokea chanjo hiyo mapema leo Ijumaa.

Taarifa hiyo imekumbusha kuwa, Kiongozi Muadhamu alipigwa dozi ya kwanza ya chanjo ya corona ya COVIran Barekat mnamo Ijumaa ya Juni 25.

Baada ya kudunga dozi ya kwanza ya chanjo ya corona ya COVIran Barekat iliyotengeneza na waatalamu wa Iran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema kuwa: Kuna ulazima wa kuthamini na kuenzi fahari hii ya taifa ya kuzalisha chanjo ya Kiirani ya corona.

Ayatullah Ali Khamenei aliwashukuru watalamu na maafisa wote walioipa nchi hii fahari ya kitaifa kutokana na elimu, tajiriba na juhudi zao kubwa za kisayansi na kivitendo na kusema: "Awali sikupendelea kutumia chanjo isiyokuwa ya Kiirani, kwa msingi huo nilisema kwamba, nitasubiri chanjo ya Kiirani ya corona; kwa sababu tunapaswa kuthamini fahari hii ya taifa.

Chanjo ya corona ya COVIran Barekat ni matunda ya wahakiki na wanasayansi vijana wa Iran ambayo hivi karibuni iliidhinishwa kuanza kutumiwa kwa ajili ya kujikingi na ugonjwa wa COVID-19.

Kuzinduliwa chanjo hiyo kunaiweka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika orodha ya nchi sita tu duniani zinazotengeneza chanjo ya corona.

342/