Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

6 Oktoba 2022

18:29:38
1311127

Trump: 'Ulimwengu unaicheka Marekani, unatutazama kwa dhihaka'

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump amesema "dunia inatucheka na inaitazama Marekani kwa dhihaka."

Trump ambaye alikuwa kihutubia wanachi katika mji wa Miami amesema: "Chini ya utawala wa Joe Biden tumekuwa nchi ya mdororo wa uchumi, pengine unyogovu, ukandamizaji, taabu na woga."

Akisisitiza haja ya serikali ya Biden kuwaomba radhi watu wa Marekani, rais huyo wa zamani wa Marekani amemkosoa vikali rais wa sasa wa nchi hiyo kwa "kuomba mafuta" na kuziomba nchi mbalimbali zizidishe uzalishaji wa bidhaa hiyo.

"Kazi inayofanywa na utawala wa Biden ni wendawazimu mtupu. Marekani imekuwa ombaomba wa mafuta kwa Venezuela na Saudi Arabia ilhali ina akiba kubwa zaidi ya mafuta", amesisitiza Donald Trump. Trump, ambaye ameshasailiwa zaidi ya mara moja bungeni na kupoteza kiti cha rais wa Marekani yake 2020, ametuma ishara kali kwamba ana mpango wa kugombea tena urais mnamo 2024.

Uchunguzi kadhaa unaendelea kuhusu rais huyo wa zamani wa Marekani, ikiwa ni pamoja na iwapo alijaribu kutengua matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2020 au la. Matokeo ya uchaguzi huo yalionesha kuwa Trump alishindwa na mpinzani wake wa chama cha Democratic, Joe Biden.

Kesi kuhusu ghasia za Januari 6, 2021 wakati wafuasi wa Trump walipovamia majengo ya Congress ya nchi hiyo na jukumu la Trump mwenyewe katika kuchochea umati wa wafuasi wake ambao walizuia kwa muda uthibitisho wa ushindi wa Joe Biden, inatarajiwa kutoa ripoti yake kabla ya kumalizika mwa huu.

Kura ya maoni ya hivi majuzi ya Yahoo News/YouGov, ilionyesha kuwa asilimia 51 ya wapiga kura waliojiandikisha wanaamini kuwa Trump hapaswi kuruhusiwa kuhudumu tena kama rais wa Marekani katika siku zijazo.


342/