Main Title

source : Parstoday
Jumatano

3 Mei 2023

10:47:50
1362350

UN yataka kufanyika uchunguzi kuhusu kifo cha Sheikh Khader Adnan

Farhan Haq Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa Antonio Guterres Katibu Mkuu wa umoja huo ametaka kufanyika uchunguzi kuhusu kufa shahidi kwa Sheikh Khader Adnan katika jela za utawala wa Kizayuni.

Farhan Haq ameeleza kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anafuatlia kwa wasiwasi matukio baada ya kufa shahidi Sheikh Adnan  na kuongeza kuwa: Guterres amewataka viongozi wa Israel kuacha mtindo wa kuwatia nguvuni watu bila ya kufunguliwa mashtaka. 

Haq ameongeza kuwa, watu wote walioko jela bila ya kufunguliwa mashtaka wanapaswa kushtakiwa au kuachiwa huru mara moja kwa mujibu wa sheria za mahakama. Sheikh Khader Adnan raia wa Palestina aliyekuwa amefungwa jela jana asubuhi alikufa shahidi akiwa katika magereza ya utawala wa Kizayuni baada ya kugoma kula kwa siku 86. 

Sheikh Adnan ni miongoni mwa watu wa awali kutoka katika kijiji cha Arabah huko Jenin ambaye alijiunga na Jihadul- Islami ya Palestina mwanzoni mwa muongo wa 80 baada ya kuasisiwa harakati hiyo; na yeye ni kati ya waasisi wa mwanzoni kabisa wa harakati ya Jihadul-Islami katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.  

Makundi ya muqawama ya Palestina yamevurumisha maroketi katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vya Sderot, Nir Am,  Ibim na Sha'ar HaNegev kufuatia kuuliwa shahidi Sheikh Khader Adnan. 

342/