7 Mei 2023 - 11:59
WHO: haiwezekani kutokomeza kabisa virusi vya Corona

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Afya Duniani anayehusika na Dharura za Kiafya ameeleza kuwa kuna vigezo maalumu sana na vya kipekee kwa ajili ya kutokomeza virusi vya corona na kwamba ni vigumu kutokomeza kabisa virusi hivyo.

Michael Rayan amesisitiza kuwa, inawezekana kuondolewa tishio la virusi vya corona dhidi ya afya ya umma kupitia utoaji chanjo na matibabu; na hivyo kuweza kuhitimisha hali ya dharura lakini hatuwezi kuviangamiza kikamilifu virusi vya corona. 

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Data Tedros Adhanom Gebreyesus pia juzi alitangaza kufikia kikomo hali ya dharura ya maambukizi ya corona. Dakta Tedros alisisitiza kuwa hii haimaanishi kumalizika tishio la virusi vya corona bali bado kuna hatari ya kubadilika upya virusi hivyo. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ametathmini kuwa hadi sasa zaidi ya watu milioni saba wameaga dunia kwa ugonjwa wa Uviko-19 duniani na kwamba kuna uwezekano takriban watu milioni 20 walikufa kwa ugonjwa huo. 

342/