Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

8 Mei 2023

10:23:47
1363773

FAO: Nchi zipatazo 60 zinakabiliwa na hali mbaya ya uhaba wa chakula wa viwango vya kutisha

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza katika ripoti yake kwamba karibu nchi 60 duniani zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na katika viwango vya kutisha.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) inaonyesha kuwa, zaidi ya watu milioni 250 katika nchi 58 duniani wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na katika viwango vya kutisha.Kulingana na ripoti hiyo ya FAO, hali mbaya ya uhaba wa chakula imeongezeka kutoka asilimia 21 mnamo mwaka 2021 hadi zaidi ya asilimia 22 katika mwaka 2022.Kutokana na kuendelea mizozo ya kivita na mapigano ya silaha katika nchi za Sudan na Ukraine, athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi pamoja na athari za janga la dunia nzima la Corona kwa uchumi wa dunia, nchi masikini duniani zinategemea zaidi uagizaji wa chakula kutoka nje ya nchi ambao gharama zake zimepanda mno kutokana na kuongezeka kwa bei ya nishati na chakula duniani.../

342/