Main Title

source : Parstoday
Jumanne

9 Mei 2023

14:28:51
1364132

Mamilioni ya hekta za ardhi ya kilimo Marekani zachafuliwa na mada za sumu

Watafiti wa Kimarekani wametahadharisha kuhusu uchafuzi wa mamilioni ya hekta za ardhi ya kilimo zilizoharibiwa na mada za sumu nchini humo.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, majaribio mapya ya kimaabara yaliyofanywa huko Marekani yanaonyesha kuwa baadhi ya viuatilifu vya chakula ambavyo vinatumika sana mashambani vimechafuliwa kwa "kiwango cha sumu ya kemikali" ambacho ni hatari kwa binadamu. 

Mada hizo ziinazojulikana kwa jina la "Persistent Chemical Substances" (PFAS) zimetajwa kuwa na uhusiano na saratani. Shirika la Kulinda Mazingira la Marekani huko nyuma lilikaa kimya kuhusu uwepo wa mada hizo za kemikali katika viuatilifu licha ya kugunduliwa kwa kemikali hizo katika bidhaa zisizo za chakula. 

Watafiti hao wametahadharisha kuhusu kuchafuliwa mamilioni ya hekta za mashamba ya kilimo huko Marekani na kutaka kuchukuliwe hatua za haraka na madhubuti  za usimamizi katika uwanja huo.

Watafiti wa Marekani wiki iliyopita walituma matokeo ya uchunguzi huo wa kimaabara kwa Shirika la Kulinda Mazingira la nchi hiyo na Idara ya Udhibiti wa Viuatilifu ya jimbo la California na kuzitaka taasisi hizo kuondoa bidhaa hizo katika kalibu ya kapu la bidhaa wanazotumia wananchi hadi hapo uchafuzi huo utakapopatiwa ufumbuzi.  

342/