Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Mei 2023

10:24:12
1364459

Wanachama wa UNSC wataka kifanyike kikao cha dharura kufuatia mashambulio dhidi ya Gaza

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kufanyika kikao cha dharura cha baraza hilo ili kujadili matukio ya Ukanda wa Gaza kufuatia mashambulio ya kinyama yaliyofanywa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Shirika la habari la Palestina la SAMA limeripoti kuwa Ufaransa na China, wanachama wawili wa kudumu wa Baraza la Usalama na Muungano wa Falme za Kiarabu ikiwa ni mwanachama asiye wa kudumu, wameomba ufanyike mkutano wa dharura leo Jumatano, ili kujadili matukio yanayojiri katika Ukanda wa Gaza na mashambulio ya kikatili yaliyofanywa hivi karibuni na utawala wa Kizayuni katika eneo hilo.

Tovuti ya chaneli ya 12 ya utawala wa Kizayuni imetangaza kuwa, viongozi wa utawala huo wanafanya juu chini ili kuzuia kufanyika mkutano huo maalumu wa Baraza la Usalama kuhusiana na matukio yanayozidi kupamba moto katika Ukanda wa Gaza; lakini hadi sasa hatua hizo zimeambulia patupu.

Siku ya Jumanne ndege za kivita za utawala haramu wa Kizayuni zilifanya mashambulio dhidi ya Ukanda wa Gaza na kuwaua shahidi Wapalestina 15 wakiwemo wanawake wanne na watoto wanne.Umoja wa Mataifa umetoa tamko la kulaani mashambulizi hayo ya kinyama ya utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.../

342/