Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

12 Mei 2023

14:36:28
1365009

Marekani haishi kulalamika, sasa yadai Afrika Kusini imeipa silaha Russia

Ikiwa ni muendelezo wa kulalamika kusikokwisha kunakofanywa na dola la kiistikbari la Marekani, balozi wa nchi hiyo huko Afrika Kusini amelalamika kuwa nchi hiyo imeipelekea Russia silaha za kijeshi.

Shirika la habari la Mehr limeinukuu News 24 ikisema kuwa, balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini amedai kuwa nchi hiyo imeipelekea silaha za kijeshi Russia na hilo kwa mtazamo wa balozi huyo, halikubaliki.

Balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, Ruben Brighetti, amedai kuwa, nchi hiyo iliipelekea Russia silaha mwezi Disemba mwaka jana kupitia meli ya Russia iliyotia nanga katika kituo cha jeshi la wanamaji cha Simmons Town mjini Cape Town.

Balozi wa Marekani mjini Cape Town amedai pia kuwa, Washington inaamini kwamba Afrika Kusini imetuma silaha nchini Russia, licha ya kwamba inadai kutoegemea upande wowote katika vita vya. Ametoa madai hayo bila ya ushahidi wowote.

Marekani ni nchi iliyo mstari wa mbele kuisheheneza silaha Ukraine kwa ajili ya kurefusha vita dhidi ya Russia. 

Hivi sasa imetoa madai hayo dhidi ya Afrika Kusini katika hali ambayo Marekani na madola ya Magharibi yanaendelea kulaumiwa kwa kuchochea moto wa vita nchini Ukraine. Madola hayo ya kibeberu ya Magharibi yanaipa serikali ya Ukraine silaha za kila namna licha ya kujua vyema kwamba wanaoathirika zaidi na vita hivyo ni wananchi wa Ukraine na ardhi ya nchi hiyo kwani kimsingi vita vinapiganwa ndani ya ardhi ya Ukraine na kamwe Russia haikubali kuchezewa mipaka yake na usalama wa taifa lake.

342/