Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

22 Mei 2023

05:04:29
1367681

Katibu Mkuu wa UN: Kutokomezwa silaha za nyuklia duniani ni jambo linalowezekana

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema katika mahojiano pembeni ya mkutano wa kilele wa Kundi la G7 huko Hiroshima, Japan kwamba inawezekana kulifikia lengo na madhumuni ya mkutano wa kilele wa kundi hilo, ambayo yametajwa kuwa ni kuwepo ulimwengu usio na silaha za nyuklia.

Mnamo Agosti 6, 1945 Marekani ilidondosha bomu la kwanza la atomiki duniani katika mji wa Hiroshima nchini Japan.Jinai hiyo iliyo dhidi ya binadamu iliyofanywa na Marekani ilisababisha kuteketezwa mji wa Hiroshima na kuuawa watu wasiopungua 140,000. Siku tatu baadaye, Marekani ilidondosha bomu la pili la atomiki kwenye mji wa Nagasaki, na kuteketeza roho za watu wengine 70,000.Kwa mujibu wa shirika la habari la Kyodo, Guterres amesema: Waziri Mkuu wa Japan Fumio Keshida amependekeza kwa usahihi mada kuu ya "kufikia ulimwengu usio na silaha za nyuklia" katika mkutano wa sasa wa G7.Miongoni mwa nchi za G7, nchi tatu ambazo ni Marekani, Ufaransa na Uingereza zina silaha za nyuklia; na nchi nyingine, yaani Italia, Canada, Japan na Ujerumani, zinaungwa mkono kuwa na silaha hizo za maangamizi.Kabla ya hapo, aliposhiriki katika kumbukumbu ya mwaka 2022 ya shambulio la bomu la atomiki nchini Japan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo pia alizihimiza nchi zote kuweka katika ajenda zao sera ya "kutotangulia kutumia" silaha za nyuklia.Itakumbukwa kuwa Jake Sullivan, mshauri wa usalama wa taifa wa Ikulu ya White House, alitamka bayana kwamba Rais wa Marekani Joe Biden hataomba msamaha kwa Japan, wakati wa ziara yake nchini humo ya kushiriki katika mkutano wa G7, kwa sababu ya mashambulio ya mabomu ya nyuklia iliyofanya nchi yake huko Hiroshima na Nagasaki.../

 342/