Main Title

source : Parstoday
Jumanne

23 Mei 2023

10:55:21
1368080

UN: Mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha vifo vya watu milioni 2

Umoja wa Mataifa umesema katika ripoti yake ya hivi karibuni kabisa kwamba, zaidi ya asilimia 90 ya vifo vinavyosababishwa na majanga duniani kote hutokea katika nchi maskini na zinazoendelea.

Ripoti hiyo imebaini kuwa zaidi ya asilimia 90 ya vifo vilivyoripotiwa duniani kote kutokana na majanga hayo vimetokea kwenye nchi maskini na zinazoendelea.

Mkuu wa shirika linaloshughulikia hali ya hewa la Umoja wa Mataifa, (WMO), Petteri Taalas amesema katika taarifa yake kwamba: Kimbunga Mocha, ambacho kilisababisha maafa nchini Myanmar na Bangladesh wiki iliyopita, ni ushahidi wa wazi wa uhakika huo. 

Lakini WMO pia imesema, kuboreshwa mifumo kutoa tahadhari ya mapema na kuratibu usimamiaji wa maafa kumepunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya binadamu.

Amesema wakati majanga kama ya kimbunga cha Mocha yalipotokea huko nyuma huko “Myanmar na Bangladesh yalisababisha vifo vya makumi bali hata mamia ya maelfu ya watu, lakini hatua zilizochukuliwa baadaye kimataifa, zinaonekana kupunguza idadi ya vifo katika majanga kama hayo.

Katika ripoti yake ya mwaka 2021 iliyoangazia vifo na hasara zilizotokana na maafa ya kibinadamu tangu 1970 hadi 2019, shirika hilo lilisema kwamba mwanzoni mwa kipindi hicho, ulimwengu ulishuhudia vifo zaidi ya 50,000 kila mwaka lakini ilipofikia miaka ya 2010, idadi ya vifo vya maafa ilipungua na kufikia chini ya 20,000 kila mwaka. 

Umoja wa Mataifa umezindua mpango wa kuhakikisha mataifa yote yanatumia mifumo ya tahadhari ya mapema ya majanga ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027. Hadi hivi sasa lakini, ni nusu tu ya nchi za dunia ndizo zilizo na mifumo hiyo.

342/