Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

27 Mei 2023

11:05:32
1369059

Sayyid Hassan Nasrullah: Hakuna tena mamlaka ya kiamri ya Marekani duniani

Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema hakuna tena mamlaka ya kiamri ya Marekani duniani na kila kitu kinaelekea kwenye ulimwengu wa kambi kadhaa, na akaongezea kwa kusema: "na hili ndilo linaloitia wasiwasi Israel".

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA; Sayyid Hassan Nasrullah ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo alipohutubia kwa mnasaba wa kumbukumbu ya ukombozi wa Lebanon, inayojulikana kama "Idi ya Muqawama na Ukombozi", na akabainisha kuwa Idi ya Muqawama inakumbusha ushindi mkubwa ilioupata Lebanon.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa: vizazi vyote na watu wa Lebanon inapasa wakumbushwe kuwa ushindi uliopatikana haukuwa wa bure, bali ni matunda na matokeo ya miaka mingi ya kujitoa mhanga.

Nasrullah ameongeza kuwa: Israel hivi sasa imejificha nyuma ya kuta na moto na haina uwezo wa kutwisha masharti yake katika mazungumzo na watu wa Palestina.

Sayyid Hassan Nasrullah ameeleza pia kuwa mkabala na mpasuko uliozuka ndani ya Israel, mshikamano na uthabiti ndio unaotawala ndani ya mhimili wa muqawama na akatanabahisha kwa kusema: "vita na adui Mzayuni havijamalizika kwani kuna sehemu ya ardhi yetu ambayo ingali inakaliwa kwa mabavu".

Halikadhalika amepongeza na kushukuru misimamo ya Iran na Syria katika kuunga mkono Muqawama na akaongeza kuwa: misimamo aliyoonyesha Ayatullah Seyed Ebrahim Raisi, rais wa Iran katika ziara yake nchini Syria baada ya miaka 12 ya vita vya dunia dhidi ya nchi hiyo inathibitisha mshikamano uliopo katika mhimili wa Muqawama.

Sayyid Hassan Nasrullah amejibu pia vitisho vya waziri mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu kwa kumwambia: "si nyinyi mnaotutishia sisi vita vikubwa, bali ni sisi tunaokutishieni nyinyi kwa vita hivyo".

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameeleza pia kwamba adui mzayuni ameweza kuanzisha uhusiano wa kawaida na baadhi ya tawala za Kiarabu, lakini hajaweza kuanzisha uhusiano wa kawaida na wananchi wa tawala hizo na akabainisha kwamba, utawala huo ghasibu umetambua kuwa tawala za Kiarabu hazina uwezo wa kuwalazimisha watu wao wakubali suala hilo.

Sayyid Hassan Nasrullah amemalizia hotuba yake kwa kusisitiza kuwa, Israel itasambaratika, na ni uhakika kwamba msambaratiko huo utatokea tu.../

342/