Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

27 Mei 2023

11:08:12
1369062

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la IRGC: Hakuna haja ya kuwepo nchi ajinabi katika Ghuba ya Uajemi

Kamanda wa kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: Iran na nchi za eneo ni wadhamini wa usalama wa Ghuba ya Uajemi na hakuna haja ya kuwepo nchi ajinabi katika eneo hili.

Kwa mujibu wa shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, Brigedia Jenerali Alireza Tangsiri, kamanda wa Jeshi la Wanamaji la IRGC amesema katika hotuba aliyotoa mjini Ahvaz katika maadhimisho ya Khordad 4, Siku ya Muqawama na Uthabiti wa Dezful ya kwamba: taifa la Iran limeimama imara mbele ya adui kwa izza, ujasiri na uthabiti na kwa hivyo Iran na nchi za eneo zinao uwezo wa kudhamini usalama wa Ghuba ya Uajemi na hakuna haja yoyote ya kuwepo nchi za kigeni katika eneo hili.

Jenerali Tangsiri amesisitiza kuwa, iwapo maadui watashambulia maslahi ya taifa la Iran baharini, jibu kali litatolewa dhidi yao. 

Halikadhalika amewaenzi mashahidi wa Dezful na mkoa wa Khuzestan na akaongezea kwa kusema: kila pale adui aliposhindwa kwenye medani ya vita, aliushambulia mji huo kwa makombora.

Kamanda wa kikosi cha wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: adui alitaka kukabiliana na muqawama wa watu wa Dezful kwa mashambulizi ya makombora, lakini kuendelea kusimama imara na kwa ujasiri watu wa mji huo kuliwafanya adui ashindwe.

Katika kalenda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, tarehe 4 Khordad (Mei 25) inajulikana kama siku ya Muqawama wa Dezful, moja ya miji ya mkoa wa Khuzestan, ulioko kusini magharibi mwa Iran.

Sababu ya siku hii kupewa jina hilo ni muqawama wa watu wa Dezful wa kuhimili na kukabiliana na hujuma na mashambulio makali na ya mtawalia ya makombora ya utawala wa Baath wa Iraq wakati wa vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala huo dhidi ya Iran.../

342/