Main Title

source : Parstoday
Jumapili

28 Mei 2023

19:54:46
1369421

Mapigano yazuka kati ya askari wa mpakani wa Iran na wapiganaji wa Taliban

Mapigano yamezuka kati ya Vikosi vya Walinzi wa Mpaka wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na vikosi vya Taliban kwenye mpaka wa Sistan na Baluchistan ya Iran na mkoa wa Nimroz wa Afghanistan, na katika maeneo mengine ya kandokando ya vijiji kadhaa ikiwa ni pamoja na Sasoli, Hatem na Makki.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, silaha nyepesi na za wastani pamoja na mizinga zilitumika katika makabiliano hayo, hata hivyo, habari kwamba majeshi ya Iran yalitumia makombora ni uongo mtupu. Kwa mujibu wa Tasnim, ripoti zilizodai kuwa uwanja wa ndege wa Zaranj nchini Afghanistan ulishambuliwa na vikosi vya Iran nazo pia hazina ukweli wowote na mapigano hayo yametokea kandokando ya maeneo ya vijiji vya Sasoli, Hatem na Makki tu. Baada ya kuanza makabiliano hayo, maandikiano na mawasiliano yalifanywa kati ya ubalozi wa Iran nchini Afghanistan na Wizara ya Ulinzi ya serikali ya Taliban. Kufuatia hatua hiyo, mapigano hayo yalimalizika; na pande mbili zimeketi kuchunguza sababu zilizopelekea kutokea mikwaruzano hiyo.../

342/