Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

2 Juni 2023

21:07:10
1370715

Rais wa Marekani Joe Biden apiga mweleka vibaya katika hafla ya Colorado

Rais Joe Biden wa Marekani alipiga mweleka na kuanguka, tukio lililoshangaza wengi, wakati wa uzinduzi wa sherehe ya vikosi vya anga vya Marekani huko Colorado.

Mara tu baada ya kumaliza hotuba yake ya uzinduzi katika mahafali ya Chuo cha Jeshi la Wanahewa la Marekani kaskazini mwa Colorado Springs, Joe Biden alijikwaa na kupiga mweleka alipokuwa akijaribu kukimbia kutoka jukwaani.

Haraka sana, askari kadhaa na wahudumu wake wa usalama walimkimbilia rais huyo wa miaka 80 ili kumsaidia kuamka na kurudi mahali pake, huku waliokuwepo katika sherehe hiyo wakipiga makofi.

Baada ya tukio hilo, rais wa Marekani alielekeza kidole kwenye sakafu ya jukwaa ambalo alisema ni chanzo chayeye kuanguka baaad aya kujikwaa.

Tukio hili la kusikitisha la Joe Biden, ambalo linaonekana kuwa si la kawaida, tayari linachochea mjadala kuhusu umri wa rais, mgombea katika uchaguzi wa urais mwaka 2024, ambao wafuasi wa Donald Trump, 76, wamekuwa wakikosoa.

Joe Biden alitangaza kugombea kwake mwishoni mwa Aprili, na kuahidi kurejesha "heshima" kwa Marekani ya wafanyakazi. Hapo awali Wamarekani hawakuwahi kumchagua rais mzee kama huyo, wala mgombea hakuwahi kuomba kura kuwania uchaguzi alipokuwa na umri wa miaka 86.

Uchunguzi wa maoni wa hivi majuzi unaonyesha kuwa wapiga kura wengi wa Marekani wana wasiwasi kuhusu umri wake mkubwa.

Kuanguka huku, pamoja na kujikwaa hapo awali kutoka kwa baiskeli yake na njiani akipanda ngazi za Air Force One, kunaweza kuongeza wasiwasi huo.

Daktari wa Ikulu ya Marekani Dkt Kevin O'Connor aliandika wakati huo: "Rais bado anastahili kuhudumu, na anatekeleza kikamilifu majukumu yake yote bila udhuru yoyote ya kila mara."

Joe Biden ambaye ana umri wa miaka 80 ndiye rais mzee zaidi katika historia ya Marekani. Amekuwa akishutumiwa mara nyingi na Warepublicans kwa kutowajibika ipasavyo mkabala wa majukumu yake kama Rais wa Marekani.


342/