Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

2 Juni 2023

21:07:40
1370716

Ayatullah Ahmad Khatami: Muqawama na uchajimungu viini viwili vya kumkwamisha adui

Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, kile ambacho kinawakwamisha maadui ni muqawama, kusimama kidete, maneno ya haki, uchajimungu na kulinda mipaka ya Mwenyezi Mungu.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema ha yoleo katika hotuba zake za Swala ya Ijumaa hapa mjini Tehran na kusisitiza kwamba, muqawama yaani kusimama kidete na uchajimungu ni viini viwili vya kumkwamisha adui.

Ayatullah Khatami ameongeza kuwa, imepita miaka 44 tangu Mapinduzi ya Kiislamu yapate ushindi hapa nchini na kwamba, siri ya mafanikio ya miaka hii 44 ni kusimama kidete katika vita vya miaka minane vya kulazimishwa Iran vilivyoanzishwa na dikteta wa wakati huo wa Iraq Saddam Hussein.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran ameashiria miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusiana na harakati za kidiplomasia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kueleza kwamba, harakati za kidiplomsia za serikali ya awamu ya 13 zilizoenekana katika kiezi ya hivi karibuni zinastahiki kupongezwa.

Ayatullah Ahmad Khatami ameashiria pia kuukaribia hauli na kumbukumbu ya kifo cha Imam Khomeini mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kueleza bayana kwamba, Imam Khomeini alikuwa na imani na wananchi na ni wananchi hawa hawa ambao walifanikiwa kuundoa madarakani utawala fisadi wa Shah na badala yake kuuweka madarakani utawala wa Kiislamu.

342/