Main Title

source : Parstoday
Jumapili

11 Februari 2024

19:15:43
1436862

Mamilioni ya Wairani waadhimisha Mapinduzi ya Kiislamu, wasema yamehuisha Umma wa Kiislamu

Mamilioni ya wananchi wa Iran walioshiriki katika maandamano ya kuadhimisha miaka 45 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini wametangaza kuwa: Mapinduzi ya Kiislamu yameibua roho mpya katika mwili wa Umma wa Kiislamu na kupanua zaidi mapambano ya kupinga dhulma na uonevu.

Hayo yameelezwa katika azimio lililotolewa mwishoni mwa maandamano makubwa ya mamilioni ya wananchi wa Iran yaliyofanyika kote nchini kuadhimisha Mapinduzi ya Kiislamu yaliyopata ushindi Februari mwaka 1979 chini ya uongozi wa Imam Ruhullah Khomeini.

Katika azimio hilo, washiriki wametangaza tena utiifu wao kwa malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Imam Ruhullah Khomeini (RA) na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameweka roho mpya katika mwili wa Umma wa Kiislamu, na sambamba na kupanua mapambano ya kupinga dhulma na nyanja za makabiliano ya kimkakati na mfumo wa kibeberu nje ya ya jiografia ya Iran ya Kiislamu, yamefungua ukurasa mpya kwa jamii ya wanadamu na kutoa bishara njema ya kujitokeza mfumo mpya wa kimataifa".

Katika azimio hilo, washiriki wameutaja umoja, mshikamano na maelewano ya kitaifa katika mhimili wa utawala wa faqihi na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kuwa ni wadhamini wakuu na vichochezi vya ushindi wa Iran ya Kiislamu kwa ajili ya kuvuka migogoro, fitna na changamoto zinazosababishwa na njama za maadui wa kigeni na watu wasiolitakia mema taifa, ndani ya nchi.Katika sehemu moja ya azimio la mwisho la waandamanaji katika maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu imeelezwa kuwa: Taifa la Iran, linathamini ushindi mtukufu na wa kihistoria wa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na kushindwa kusikoweza kurekebishwa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, na linayatambua masaibu ya sasa huko Gaza kuwa ni masaibu ya ubinadamu yanayoonyesha kubatilika na kufeli mfumo wa sasa wa dunia.

Vilevile limelaani mauaji ya kimbari yanayofanywa na Wazayuni huko Gaza kwa himaya na uungaji mkono usio na kikomo na wa pande zote wa Marekani mtendajinai, na kupongeza uungaji mkono wa kimataifa kwa watu wa Gaza na wapigania ukombozi wa Palestina.

Azimio lililotolewa na mamilioni ya waandamanaji katika maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran pia limezitaka nchi za Kiislamu kutekeleza matakwa ya Umma wa Kiislamu ya kujiepusha na aina yoyote ya uungaji mkono na msaada kwa utawala bandia, wa Kizayuni na wenye sifa za mbwa mwitu wa Israel, na kutoa kipigo kikubwa kwa utawala huo ulioivamia Palestina na kuikalia kwa mabavu Al-Quds, kwa kukata uhusiano wa kiuchumi. Vilevile wamesisitiza kuwa: Taifa la Iran linaitaka jamii ya kimataifa ifute uanachama wa utawala bandia wa Israel unaoua watoto, na kuwatimua wawakilishi na mabalozi wa utawala huo katika Umoja wa Mataifa kutokana na uhalifu wa mauaji ya kimbari, ukatili na maangamizi ya kizazi yanayofanywa na utawala huo huko Palestina. 

342/