"Shukran kwa Mwenyezi Mungu, hii ni siku nzuri; siku ya ushiriki na kuhusika athirifu watu wetu wapendwa katika tukio muhimu la kitaifa; yaani uchaguzi," amesema Ayatullah Khamenei baada ya kupiga kura yake katika kituo cha kupigia kura mjini Tehran.
"Nimesikia kwamba shauku na hamasa ya wananchi ni ya juu zaidi kuliko ile iliyoshuhudiwa katika duru ya kwanza. Mwenyezi Mungu ajaalie hivyo, na ikiwa itakuwa hivyo, itakuwa ya kuridhisha," amesisitiza Ayatullah Khamenei.Maeneo ya kupigia kura yamefunguliwa asubuhi saa mbili kamili na yatafungwa saa kumi na mbili jioni. Wizara ya Mambo ya Ndani inaweza kuongeza muda huo iwapo itahitajika.
Uchaguzi wa marudio unafanyika kwa sababu hakuna mgombeaji aliyepata wingi wa wazi wa kura katika uchaguzi wa Ijumaa iliyopita, Juni 28.
Veterani wa vita vya Saddam Hussein dhidi ya Iran, Saeed Jalili, ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa na kiongozi wa timu ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia na nchi za Magharibi, anachuana na waziri wa zamani wa afya, Daktari Masoud Pezeshkian. Wawili hawa walipata kura nyingi zaidi katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Iran Ijumaa iliyopita.
342/