Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

6 Julai 2024

16:34:15
1470011

Kiongozi Muadhamu ampongeza Rais mteule wa Iran; awashukuru Wairani kwa kupiga kura kwa wingi

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amempongeza Rais mteule wa Iran, Masoud Pezeshkian na kutoa shukrani za dhati pia kwa wagombea wote wa uchaguzi wa 14 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu; na maafisa walioshiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi huo.

Katika ujumbe wake leo Jumamosi, Ayatullah Ali Khamenei ameashiria haja ya Rais mteule kutumia uwezo wa nchi kwa ajili ya ustawi wa watu na maendeleo ya nchi na kusema, "Pia ninamshauri Rais mteule Dakta Pezeshkian kutazamia upeo wa mustakabali mzuri akiwa na matumaini kwa Allah, na kuendeleza njia ya Shahidi (Ibrahim) Raisi ya kuwapa faraja wananchi na haswa vijana, wanamapinduzi na waaminifu, kwa kutumia rasilimali na uwezo wote wa nchi."

Kadhalika Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema ushiriki mkubwa wa Wairani katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais umelipa fahari taifa la Iran sambamba na kuwaghadhabisha maadui wa Jamhuri ya Kiislamu waliofanya kampeni kubwa ya kutaka zoezi hilo lisusiwe.

Ayatullah Sayyid Khamenei ameeleza bayana kuwa, ushiriki mkubwa na wenye hamasa wa taifa katika uchaguzi wa jana ni dhihirisho la nguvu ya kitaifa, na kwamba ushiriki huo wa kishindo umewakatisha tamaa maadui wa Iran. 

Amebainisha kuwa: Hatua hii adhimu ya kukabiliana na suitofahamu iliyotengenezwa ya kususia uchaguzi, ambayo maadui wa taifa la Iran walikuwa wameianzisha ili kuzusha hali ya kukata tamaa na mkwamo (nchini), ni kazi nzuri na isiyoweza kusahaulika."

Kadhalika Ayatullah Khemenei amewapongeza wagombea wote waheshimiwa na wale wote waliofanya kazi usiku na mchana kwa wiki kadhaa kufanikisha uchaguzi huo akisisitiza kuwa wamelipa heshima na izza taifa hili. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kuwa, "Sasa kwa kuwa taifa la Iran limeshamchagua rais wake, nalipongeza taifa na Rais mteule, na wote wanaofanya kazi katika kipindi hiki nyeti na hasasi, hasa vijana wenye shauku katika Makao Makuu ya Uchaguzi, na ninapendekeza kila mtu atoe ushirikiano na kutafakari juu ya maendeleo na kuongeza heshima ya nchi.”

342/