Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

6 Julai 2024

16:35:15
1470013

Kiongozi wa Mapinduzi: Suala muhimu zaidi la sasa ni kushindwa nchi za Magharibi kimaadili na kisiasa

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa suala muhimu zaidi duniani leo hii ni kufeli nchi za Magharibi katika masuala ya kimaadili na kisiasa.

Katika ujumbe wake uliosomwa kwenye Mkutano wa 58 wa Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu barani Ulaya, Ayatullah Ali Khamenei ameashiria matukio ya Gaza na maafa ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel katika eneo hilo la Palestina na kusema: Suala muhimu zaidi leo hii duniani ni kushindwa kimaadili, kisiasa na kijamii nchi za Magharibi na wanasiasa wa nchi hizo na vilevile utamaduni wa Kimagharibi.  

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Maafa yenye kutoa ibra zaidi ni kutokuwa na uwezo demokrasia ya Kiliberali wa kuanzisha uhuru wa kujieleza, na kupuuza kwao vibaya suala la uadilifu wa kiuchumi na kijamii. Amesema, cheche hafifu lakini imayotia matumaini ya maandamano ya wananchi hususan wanafunzi wa vyuo vikuu huko Marekani na barani Ulaya ni mojawapo ya masuala muhimu zaidi ya kipindi cha sasa. 

Ayatullah Khamenei pia ameashiria masuala nyeti ya sasa ya dunia na kusisitiza udharura wa mchango muhimu na athirifu wa wanafunzi wa vyuo vikuu katika masuala makubwa kwa kutegemea irada, imani na kujiamini.  

342/