Massoud Pezeshkian ameibuka na ushindi baada ya kupata kura milioni 16 na 384,403 kati ya jumla ya kura milioni 30 na 530,157 zlizopigwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Iran uliofanyika jana kote nchini.
Shirika la Habari la Iran (IRNA) limeripoti kuwa, Narendra Modi Waziri Mkuu wa India amepongeza ushindi wa Massoud Pezeshkian na kusema kuimarisha zaidi uhusiano mwema wa pande mbili na wa muda mrefu kuna maslahi ya wananchi na eneo kwa ujumla.
Waziri Mkuu wa Malaysia, Naye Anwar Ibrahim, amempongeza Dakta Massoud Pezeshkian kwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa Rais wa Iranna kusema kuwa ushindi huu ni bishara njema kwa Iran.
Amir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na Sultan wa Oman Haitham bin Tariq pia wamemtumia jumbe tofauti rais mteule Massoud Pezeshkian wakimpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Iran.
Wakati huo huo Amir wa Kuwait, Shekh Meshal Al Ahmad al Jabir al Sabah, pia amemtumia ujumbe wa pongezi rais mteule Massoud Pezeshkian na kumtakia kila la kheri yeye pamoja na wananchi wa Iran. Mfalme wa Bahrain, Hamad bin Issa Al Khalifa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea ya Kusini, Rais Xi Jin Ping wa China, na Rais Alexander Vucic wa Serbia pia wametuma salamu zao za pongezi kwa rais mteule wa Iran.
342/