8 Julai 2024 - 15:13
Idadi ya Mashahidi katika Ukanda wa Gaza imefikia watu elfu 38,193

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuongezeka kwa idadi ya Mashahidi wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na kufikia watu elfu 38 na 193.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imesema katika ripoti yake ya hivi punde kwamba:

Utawala wa Kizayuni umefanya mauaji mara 3 dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita, ikiwa ni mauaji ya kimbari, ambapo matokeo yake watu 40 waliuawa kishahidi, na watu wengine 75 kujeruhiwa.

Pamoja na idadi hiyo, idadi ya Mashahidi huko Gaza tangu Oktoba 7, 2023 (15 Mehr 1402) na tangu kuanza kwa operesheni ya "Kimbunga cha Al-Aqsa" mpaka sasa, imefikia watu elfu 38,193; na idadi ya watu waliojeruhiwa imefikia elfu 87,903.