Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

26 Julai 2024

17:06:45
1474555

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Rais mteule wa Iran ametokana na kura za wananchi

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema, rais mteule wa Iran amechaguliwa kwa kura za wananchi.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, Hujatul-Islam Wal-Muslimin Kazem Seddiqi, Khatibu na Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesisitiza pia kwamba mawaziri na wajumbe wa baraza jipya la mawaziri wanapaswa wawe watu wenye imani ya dhati juu ya Mfumo wa utawala; na si kuwa na unafiki kwa kusema tunaukubali lakini misimamo yao ikawa inakwenda kinyume na misingi ya Mapinduzi na Mfumo.Akizungumzia miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul-Islam Seddiqi amesema: Kiongozi wa Mapinduzi ametoa ushauri mahsusi kuhusiana na uundaji wa Baraza la Mawaziri na uteuzi wa mawaziri, na alivyopendekeza ni kwamba kabla Rais hajawasilisha bungeni majina ya mawaziri, kwanza awatathmini vizuri watu hao. 

 Sambamba na kusisitiza ulazima wa kuwepo ushirikiano baina ya Mihimili Mitatu ya Dola (Serikali, Bunge na Mahakama), ili kuweza kushughulikia matakwa ya wananchi, Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amependekeza iundwe kamati ya pamoja ya mihimili hiyo mitatu ili kuelewa masuala na matatizo ya nchi na kuweza kusaidiana pamoja kutatua matatizo hayo ya nchi na wananchi.../

342/