نatika mazungumzo ya simu na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel siku ya Jumapili, Rais Pezeshkian alisema utawala wa Israel hivi sasa unatoa vitisho zaidi kwa amani na usalama wa kieneo na kimataifa.
Ameendelea kusema kwamba:"Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa ikiunga mkono amani, utulivu na uthabiti duniani kote na inaamini kwamba mwelekeo wowote katika sehemu yoyote ya dunia unaohatarisha maadili haya unapaswa kukomeshwa."
Rais Pezeshkian amesema hayo siku moja baada ya mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Israel dhidi ya shule inayohifadhi watu waliokimbia makazi yao mashariki mwa Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya zaidi ya raia 100.
Ofisi ya vyombo vya habari vya serikali ya Gaza imesema zaidi ya raia 100 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa Jumamosi asubuhi wakiwa katika swala ya alfajiri baada ya vikosi vya Israel kushambulia kwa bomu shule ya al-Tabi'in katika kitongoji cha al-Daraj katika Jiji la Gaza.
Ukiungwa mkono na Marekani na waitifaki wake wa Magharibi, utawala ghasibu wa Israel ulianzisha uvamizi wa kila upande eneo la Gaza baada ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyotelekezwa mwezi Oktoba mwaka jana na makundi ya Palestina ambayo yalikuwa yanalipiza kisasi jinai za miongo kadhaa za Israel dhidi ya Wapalestina..
Takriban Wapalestina 40,000 wameuawa tangu wakati huo, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na wengine zaidi ya 92,000 kujeruhiwa katika uvamizi huo usio na huruma wa Israel.
342/