Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la "Wafa" la Palestina, katika taarifa hiyo pia inaelezwa kuwa idara ya kijasusi ya Kizayuni ilimwita mhubiri wa Msikiti wa al-Aqsa katika tawi la nne la kituo cha Al-Maskubiya kilichopo Jerusalem inayokaliwa kwa mabavu kwa ajili ya uchunguzi na mahojiano mida ya saa tatu alfajiri.
Hapo awali, Polisi wa Kizayuni walikuwa wameamua kumzuia Mhubiri wa Msikiti wa Al-Aqsa kuingia katika Msikiti huu na viwanja vyake kwa muda wa miezi 6 kwa sababu ya hotuba yake na maombolezo ya Shahidi Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas, ambaye aliuawa tarehe 31 Julai Mjini Tehran.
Kuhusiana na hilo, Mashahidi wa tukio hilo wameripoti juu ya shambulio la makumi ya walowezi wa Kizayuni katika eneo la Msikiti wa Al-Aqsa katika mji unaokaliwa kwa mabavu wa Quds chini ya ulinzi wa Polisi wa utawala huo ghasibu wa Kizayuni.
Walioshuhudia pia walitangaza kwamba walowezi hao wa Kizayuni walifanya doria za uchochezi na uchokozi katika Msikiti wa Al-Aqsa na kufanya sherehe zao za Talmudi katika majengo yake.