“Tabia au shakhsia yake inachangia katika kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya Waislamu na Wakristo,” aliongeza.
Katika hotuba yake, Ayatullah Moballeghi alifafanua kuhusu tabia ya Bibi Maryam (SA) kwa msingi wa Qur'an'.
“Bibi Maryam (SA) ni kama daraja la usafi na imani kati ya Uislamu na Ukristo na anachukuliwa kama alama ya utakasifu na uadilifu duniani,” alisema, akiongeza, “Hadhrat Maryam (SA) anatambuliwa kama mfano wa uchaji Mungu na maadili mema kati ya wanawake wote duniani, na maisha yake yamejaa ishara za Kimungu na miujiza ambayo yamemfanya kuwa daraja la kuleta Uislamu na Ukristo pamoja.”
Bibi Maryam (SA) ana "nafasi ya juu" katika Uislamu na Ukristo, alisisitiza msomi huyo, akitaja kuwa jina lake limetajwa mara 34 katika Qur'ani Tukufu, na Surah nzima imetengwa kwa ajili yake, ikionyesha fadhila zake adhimu.
“Maisha ya Bibi Maryam (SA) yana miujiza na ishara za kimungu, kama kupata mimba kimuujiza bila kuingiliwa na kibinadamu, riziki ya kimungu, na kuzungumza kwa Nabii Isa (AS) akiwa mtoto mchanga, akithibitisha unabii wake na Tauhidi au itikadi ya Mungu Mmoja,” alisema.
Mtazamo wa pamoja kuhusu Bibi Maryam na Bibi Fatimah (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao) unafungua njia mpya ya umoja kati ya dini, aliongeza.
Kongamano hilo liliratibiwa kwa ushirikiano na Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO).
chanzo: IQNA