20 Septemba 2024 - 20:16
Ujumbe wa Lebanon Umoja wa Mataifa: Vifaa vya mawasiliano vilitegwa mada za milipuko kabla ya kuwasili nchini

Uchunguzi wa awali uliofanywa na serikali ya Lebanon umeonyesha kuwa vifaa vya mawasiliano vilivyolipuka wiki hii nchini humo na kuua makumi ya watu "vilitengwa mada za milipuko kabla ya kuwasili Lebanon."

Ujumbe wa Lebanon katika Umoja wa Mataifa umesema uchunguzi wa awali wa serikali ya nchi hiyo umebaini kuwa, vifaa vya mawasiliano vilivyolipuka wiki hii "vilikuwa vimetengwa mada za milipuko" kabla ya kuingia nchini.

Barua iliyotumwa na Ofisi ya Mwakilishi wa Lebanon kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kabla ya mkutano uliopangwa kufanyika leo Ijumaa kuhusu suala hilo, imesema kwamba "uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa vifaa vilivyolengwa vilitegwa mada za milipuko kwa njia ya kitaalamu kabla ya kuwasili Lebanon."

Kwa mujibu wa barua hiyo, serikali ya Lebanon pia imehitimisha kuwa vifaa hivyo vya mawasiliano - ambavyo vilijumuisha pager na vifaa vingine vya mawasiliano visivyo na waya (walkie-talkies) - vililipuliwa kwa kutuma ujumbe wa kielektroniki kwa vifaa hivyo. Ujumbe huo umeongeza kuwa, Israel ndiyo iliyopanga na kutekeleza mashambulizi hayo.

Watu 37 waliuawa na karibu wengine 3,000 walijeruhiwa kutokana na milipuko ya vifaa vya kiraia vya mawasiliano siku ya Jumanne na kisha milipuko ya Jumatano vifaa vya mawasiliano visivyo na waya vilivyokuwa vikitumiwa na baadhi ya wanachama wa Hibzullah na raia wa kawaida.

Vifaa hivyo vililipuka wakati watumiaji wake wakifanya manunuzi madukani, wakitembea barabarani au kuhudhuria mazishi na shughuli nyingine za kawaida, hali iliyozusha ya taharuki nchini Lebanon.

Ujumbe wa Lebanon katika Umoja wa Mataifa umeitaja milipuko hiyo kuwa "ni ukatili usiyo na kifani"unaodhoofisha juhudi za kidiplomasia za kusitisha mapigano huko Gaza na kusini mwa Lebanon.

\342