7 Oktoba 2024 - 15:27
Tweet ya Kauli za Kiongozi kwa Lugha ya Kiebrania: Operesheni ya "Kimbunga cha al-Aqsa" imeurudisha nyuma kwa miaka 70 Utawala Haram wa Kizayuni

Katika saa za mapema za kumbukumbu ya kutimia kwa mwaka wa kwanza wa Operesheni ya (dhoruba au) "Kimbunga cha Al-Aqsa", Tweet ya Kiebrania kutoka katika maelezo ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ilichapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani ukiitwa mtandao wa Twitter) ikiwa na mada ifuatayo: "Operesheni ya dhoruba ya Al-Aqsa imeurudisha nyuma Utawala wa Kizayuni kwa miaka 70."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Sambamba na kuanza kwa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kwa mwaka uliopita, vyombo vya Habari vya KHAMENEI.IR vilichapisha maelezo (kauli au taarifa) ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Khamenei kwa Lugha ya Kiebrania kwenye Ukurasa wake wa Twitter (X) kama ifuatavyo:

"Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imeurudisha nyuma kwa miaka 70 Utawala wa Kizayuni".

Inapaswa kusemwa kuwa Muqawamah wa Palestina unaoongozwa na Hamas ulianzisha Operesheni ya kushtukiza ya kipekee kabisa alfajiri ya tarehe 7 Oktoba 2023 (15 Mehr 1402 Hijria-Shamsiyya) kwa kushambulia vitongoji vya walowezi wa Kizayuni karibu na Ghaza na walifanikiwa kuteka makumi ya Wazayuni kupipitia kudhibiti kambi kadhaa za jeshi la Israel.

Licha ya kukaguliwa (na kuminywa kwa) habari za kuuawa wanajeshi wa Kizayuni katika vita vya Ghaza, Wazayuni wenyewe wamekiri kuwa tangu tarehe 7 Oktoba mwaka jana, wanajeshi 4576 wa Kizayuni wamejeruhiwa vibaya mno, ambapo 696 kati yao wako katika hali mbaya zaidi.