Main Title

source :
Jumamosi

19 Machi 2011

20:30:00
277012

Falsafa ya Kiislam

Falsafa sehemu ya pili Na:H.Katundu

Neno fasalfa si neno geni, kwani tumekuwa tukilisikia au kilitumia mara kwa mara katika mazungumzo yetu ya kila siku. Katika mada hii nitaelezea elimu ya Falsafa muhtasari. Neno Falsafa, linatokana na neno la kigiriki PHILOSOPHIA. Ambapo ni muunganiko wa maneno mawawili: PHILO na SOPHIA. Neno PHILO linamaanisha Upendo na neno SOPHIA lina maansiha hekima.

Katika mada iliopita tulielezea maana ya kilugha ya neno Falsafa na historia ya neno hilo kwa ufupi. Katika mada hii tutaelezea maana ya falsafa katika Istilahi za kielimu.1.ISTILAHI YA WAISLAMU     Katika istilahi ya waislamu hapo kabla, neno falsafa halikumaanisha fani au elimu maalumu tu, bali lilishamilisha kila aina ya masomo ya kiakili hivyo basi kwa mujibu wa istilahi hii Mwanafalsafa alikuwa ni mtu mwenye utambuzi wa masomo ya kiakili kwa  mfano: Mantiki, Hesabati, Uhandisi, Siasa na nk. wanazuoni wa kiislam waliigawanya falsafa  katika makundi mawili:I.Falsafa ya NadhariaII.Falsafa ya matendoFalsafa ya Nadharia: inaongelea Vyanzo wa kuwepo na sababu zake pia ukweli na uhakika wa mambo.Falsafa ya matendo: inaongelea matendo ya mwanadamu na jinsi yanavyotakiwa kuwa.   Falsafa ya Nadharia imegawanyika sehemu tatu:I.Falsafa ya juu au (Metaphysics): ambayo inazungumzia mambo yanayomhusu Mwenyezi Mungu na uhakika wa mambo yasiyo maada.II.Falsafa ya kati: ambayo inazungumzia Hesabati, uhandisi , Maumbo na Muziki.III.Falsafa ya chini: ambayo inazungumzia mazingira.Falsafa ya matendo pia inavigawanyo tofauti kama vile elimu ya Maadili,Siasa...nk.Tanbihi: kunabaadhi ya wanazuoni wakubwa katika uislamu, wanapinga  masomo  mfano wa Falsafa,Kalaam na Matinki. Na wengine wakatokea hata kuharamisha masomo haya. Watu hawa ni maarufu kwa jina la Ahlul Hadith.        2.FALSAFA KATIKA ISTILAHI YA SASA.Katika istilahi ya sasa falsafa hutambulika kama: elimu inayozungumzia vyanzo, sababu na uhakika wa mambo au uhakika wa ulimwengu kwa ujumla, kwa kutumia akili bila kuelemea katika upande wowote. Hivyo basi Falsafa inalenga na kuelezea ukweli na uhakika wa mambo kwa ujumla pia inachunguza sababu na vyanzo vya ulimwengu kwa ujumla.   Kwa lugha rahisi tunaweza sema kuwa: Falsafa humtanabaisha mtu kujua yeye ni nani? ametoka wapi? Yupo wapi? yupo kwa ajili gani? anakwenda wapi? Ni njia ipi sahihi kuitumia ili kulifikia lengo lake?   Kwa minajiri hiyo basi falsafa hatuwezi kuiweka mbali na dini kwani dini pia humtanabaisha mtu kujua yeye ni nani? ametoka wapi? Yupo wapi? Kwanini yupo hapo alipo? Anakwenda wapi? Ni njia ipi sahihi kuitumia ili kufikia Lengo Lake?Tofauti ni kwamba mwanafalsafa anategemea akili pekee kufika katika malengo yake. Na mwanadini anategemea maandiko na akili. Ndugu msomaji nataraji utakuwa umestafidi na muhtasari huu.tusubiri mada itayokuja itazungumzia nini.Ahsanten