Main Title

source : ABNA
Ijumaa

7 Oktoba 2016

20:31:36
784113

Kiongozi mmoja wa Nigeria aitaka serikali ya Nigeria kufunga ubalozi wa Iran nchini humo

Mkurugenzi mkuu wa tovuti ya Suluhu nchini Nigeria ameviomba vyombo vya usalama nchini humo kuufungia ubalozi wa Iran katika mji mkuu wa nchi hiyo, hatimaye kufanya uchunguzi kuhusu balozi wa zamani wa Iran nchini humo kwa madai kuwa alikuwa anaingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Alphonse Ukemeh mkurugenzi mkuu wa tovuti ya suluhu ya kitaifa nchini Nigeria katika maelezo yake amesema akimtuhumu balozi wa Iran aliopita nchini humo kuwa anaingilia mambo ya nchi  hiyo, hivyo basi ameiomba serikali ya Nigeria kufunga ubalozi wa Iran uliopo katika mji mkuu wa nchi hiyo “Abuja”.
Alphonse Ukemeh katika kauli yake kumtuhumu balozi wa zamani wa Iran nchini Nigeria amesema kuwa balozi huyo ndiye aliyesababisha machafuko ya Nigeria ambayo yalipelekea kutokea machafuko baina ya kikundi cha harakati ya Kiislamu nchini humo na majeshi ya nchi hiyo mnamo mwezi Desemba mwaka 2015.
Mkurugenzi mkuu huyo amevitaka vyombo vya usalama nchini humo kufanya uchunguzi kuhusu balozi huyo, huku kwa upande mwingine ametaka kuufungwa kwa ubalozi wa Iran nchini humo.
Shirika la habari la Nigeria limedai kuwa kubadilishwa kwa balozi huyo na kuletwa balozi mpya nchini humo, ni ishara inayoonyesha juhudi za serikali ya Rouhani katika kuficha maovu ya balozi aliopita, kitu kitaifanya serikali ya Nigeria kushindwa kufanya uchunguzi kuhusu balozi huyo.
Tovuti hiyo imeandika kuwa “Wanigeria hawako tayari kuendeleza uhusiano wao rasmi na Iran kupitia ubalozi wa Iran nchini humo, kwa maana ubalozi wa Iran unapaswa ufungwe nakusitisha mahusiano ya Kidiplomasia na Iran, kwani kama balozi aliyepita alisababisha machafuko hayo, ni jambo lisioshindikana kwa balozi mwingine kufanya hivyo”
Hii ni katika hali ambayo vyombo vya habari mbalimbali vimetangaza kuwa ugaidi uliopo dunia unaletwa na tawala za kimarekani na Ulaya, ama shirika la habari la Nigeria ladai kuwa Iran ndio ilioasisi kikundi cha Daesh na ugaidi duniani.
mwisho wa Habari/290