Kihistoria
-
Ayatollah Khatami: Trump na Netanyahu Hawatakuwa na Usingizi wa Amani
Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Elimu ya Kiislamu ya Qom amesema kuwa ibada za mazishi ya Kiongozi aliyefariki akiwa shahidi katika maeneo mbalimbali ya nchi zimegeuka kuwa jukwaa la umoja, mshikamano na kuhuisha ahadi ya utii kwa Mapinduzi ya Kiislamu. Amesisitiza kwamba: “Trump na Netanyahu hawatakuwa na usingizi wa amani.”
-
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran: Tumeanza Enzi Mpya Chini ya Uongozi wa Ayatollah Sayyid Mojtaba Khamenei
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Aref, amesema Jamhuri ya Kiislamu imeanza enzi mpya chini ya uongozi wa Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, akitoa shukrani kwa mahudhurio makubwa ya wananchi wa Iran na Umma wa Kiislamu katika mazishi ya Kiongozi Shahidi.
-
Hilali Nyekundu: Hakuna Majeruhi Walioripotiwa Katika Hafla ya Kuaga Kiongozi Shahidi Licha ya Mamilioni ya Waombolezaji Kushiriki
Shirika la Hilali Nyekundu limetangaza kuwa hadi sasa hakuna majeruhi walioripotiwa katika hafla ya kuaga Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, licha ya mamilioni ya waombolezaji kushiriki. Shirika hilo limeeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na usimamizi mzuri wa tukio hilo pamoja na ushirikiano wa wananchi.
-
Iraq Yajitayarisha kwa Mazishi ya Kihistoria na ya Mamilioni ya Waombolezaji kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, kufuatia kuuawa shahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei, na kutokana na maombi ya mara kwa mara ya wanazuoni, viongozi wa makabila na wasomi wa Iraq, miji mitakatifu ya Najaf na Karbala inajiandaa kupokea mamilioni ya waombolezaji katika mazishi ya kihistoria yatakayofanyika tarehe 8 Julai.
-
Kaimu Waziri wa Ulinzi Iran: Taifa Limeshinda Kihistoria Dhidi ya Maadui Wake
Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema kuwa wananchi wa Iran, kwa uungwaji mkono wa vikosi vya jeshi, wamefanikiwa kuwalazimisha maadui kupata “ushindi wa kihistoria”, akisisitiza pia umuhimu wa kuimarisha umoja wa Waislamu kupitia Eid al-Adha na msimu wa Hija.
-
Leo Katika Historia:Iran Ilishambulia Kambi ya Ain al-Asad ya Marekani kwa Makombora ya Balistiki Ikiwa Kisasi cha Kuuawa kwa Jenerali Qasim Soleimani
Ilikuwa Januari 8, 2020 pindi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilipofanya Shambulizi kubwa la Kihistoria kwa kuitwanga Kambi ya Kijeshi ya Marekani iliyoitwa "Ain al-Asad" ikiwa ni sehemu ya kulipiza kiasi baada ya Kuuawa kwa Shahidi Qassem Soleimani
-
Jeshi la Lebanon liliwaruhusu waandishi wa habari kuingia katika vituo vya Hizbullah;
JKituo cha kihistoria cha Muqawama ambacho ukweli wake umejulikana baada ya kusitishwa kwa mapigano
Bonde la Zabqin, kutokana na muundo wake maalum wa kijiografia na umbali wa takribani kilomita 10 kutoka mpaka wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, linachukuliwa kuwa mojawapo ya ngome kuu za Muqawama (Upinzani). Ni ngome ambayo vizazi mbalimbali vya wapiganaji wa Kipalestina na Wenyeji wa Lebanon wamekuwa wakikuwapo humo kwa miaka mingi.
-
Kumbukumbu ya Mirza Kuchak Jangali Yapasa Kuwa Zaidi ya Sherehe ya Kihistoria
Gavana wa Gilan: “Maadhimisho ya kihistoria hayapaswi kubaki kuwa hafla za alama pekee; kumbukumbu ya Mirza Kuchak ni fursa ya kutathmini kama bado tupo katika njia ya malengo yake ya uhuru na haki.”
-
Irani Dhidi ya Magharibi: Kutoka Uzoefu wa Kihistoria Hadi Mapambano ya Kistaarabu ya Leo
Mkutano “Sisi na Magharibi katika Mitazamo na Fikra za Ayatullah Al-Udhma Sayyid Ali Khamenei” wafanyika Tehran.
-
Tamasha la Kimataifa la Filamu za Muqawama la 19 kuelekea kuwa la kimataifa – ndoto ya kufanyika kwake katika mji wa Quds Tukufu
Lengo la si tu kufanya tamasha la filamu, bali kujenga fikra na mwelekeo wa kimataifa wa sanaa ya muqawama. Tuna ndoto ya siku ambayo tamasha hili halitafanyika tena Tehran, bali katika mji wa Quds Tukufu, pamoja na watu wa Palestina walio huru. Tamasha hili limepata pumzi yake kutoka Gaza, Lebanon, Syria, Yemen na kila uwanja wa muqawama – na litaendelea hadi kufikiwa kwa ukombozi kamili wa Quds.”
-
Afisa wa Kijeshi wa Iraq: Kamwe Haitatokea kusahau msaada wa Iran
Rais wa Chuo cha Ulinzi wa Iran: “Tunafurahia sana kwamba maafisa wa Iraq wanasoma katika Chuo cha Uongozi na Makao Makuu ya Jeshi la Iran. Ingawa kuna uwezekano wa kusoma katika nchi nyingine, tunapendelea maafisa wetu wapate elimu yao hapa Iran, kwa kuwa tunajua wanapata mafunzo bora chini ya wakufunzi wenye kiwango cha juu cha kielimu na kitaaluma.”