Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kaimu Waziri wa Ulinzi na Uungaji Mkono wa Vikosi vya Jeshi la Iran amesema kuwa wananchi wa Iran wamefanikiwa kuwalazimisha maadui kushindwa na wao kupata “ushindi wa kihistoria”, akisisitiza kuwa taifa hilo limesimama imara dhidi ya mashambulizi ya kijeshi yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Katika taarifa yake, waziri huyo amebainisha kuwa Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na uungwaji mkono wa wananchi pamoja na mataifa yanayoipinga dhulma, vimeweza kukabiliana na kile alichokiita hujuma za maadui na kudhihirisha nguvu ya taifa hilo.
Aidha, amewasilisha salamu za Eid al-Adha kwa mawaziri wa ulinzi wa nchi za Kiislamu, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano kati ya mataifa ya Kiislamu katika kukabiliana na changamoto za pamoja.
Katika ujumbe wake wa Eid, ameeleza kuwa sikukuu hiyo ni ishara ya utii kwa amri za Mwenyezi Mungu na mapambano dhidi ya uovu, akiongeza kuwa msimu wa Hija unapaswa kuwa chachu ya kuimarisha undugu na mshikamano wa Umma wa Kiislamu duniani kote.
Your Comment