azimio
-
Chuo Kikuu cha Campinas, Brazil, Chataka Kukomeshwa kwa “Mauaji ya Kimbari Gaza”
Baraza Kuu la Chuo Kikuu cha Jimbo la Campinas (Consu – Unicamp) katika kikao chake cha Jumanne, Agosti 5, 2025, limepitisha azimio linalotaka kukomeshwa kwa kile walichokiita “mauaji ya kimbari Gaza” na kulitaka Serikali ya Brazil kusitisha uhusiano wake wa kibiashara na kijeshi na Israel.
-
Msimamo Mkali wa Hizbullah Dhidi ya Jaribio la Kuvunjwa kwa Silaha za Muqawama: Azimio Jipya la Serikali ya Nawaf Salam ni Tishio kwa Uhuru wa Lebanon
Chama cha Hizbullah kimetoa tamko kali kupinga uamuzi mpya wa serikali inayoongozwa na Nawaf Salam, ambao wanauona kama hatua ya hatari ya kudhoofisha muqawama (mapambano ya ukombozi) na kukabidhi usalama wa Lebanon kwa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. Katika taarifa hiyo, Hizbullah imesisitiza kuwa itakabiliana na uamuzi huu kwa msimamo thabiti kama hatua isiyokubalika kabisa, huku ikisisitiza umuhimu wa kulinda silaha za kujihami na kuimarisha jeshi la taifa kwa ajili ya kutetea ardhi na uhuru wa Lebanon. Lebanon Bado Chini ya Vitisho vya Israel na Marekani
-
Radiamali ya Wapalestina kuhusu Kura ya Veto juu ya Azimio la Baraza la Usalama: Hatua ya Marekani ni Kutoa Uhalali wa Mauaji ya Kimbari huko Gaza
Ofisi ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imelaani vikali kura ya veto iliyowekwa na Marekani dhidi ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuitaja kama ishara ya wazi ya uungaji mkono wa Washington kwa uhalifu unaotekelezwa na utawala wa Kizayuni. Taasisi hiyo imesisitiza kuwa hatua hiyo itaongeza mgogoro wa kibinadamu huko Gaza na kusababisha kuongezeka kwa mauaji ya raia wasio na hatia. Imeyataka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti ili kuokoa maisha ya watu wasiokuwa na hatia katika eneo hilo.