Shirika la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya Chuo Kikuu cha Jimbo la Campinas, kikao hicho cha asubuhi ya Jumanne, 5 Agosti 2025 (sawa na 14 Mordad 1404 kwa kalenda ya Kiajemi), kilipitisha azimio hilo likieleza kuwa vitendo vya Israel huko Gaza ni “vya uharibifu” na “ukatili unaoongezeka.” Azimio hilo limeonya kuwa ukimya mbele ya hali hiyo ya maafa unaweza kufasiriwa kama “ushirikiano”.
Katika azimio hilo, lililopewa jina “Azimio la Kukomesha Mauaji ya Kimbari Gaza na Kusaidia Kusitishwa kwa Mahusiano ya Kibiashara na Kijeshi kati ya Serikali ya Brazil na Serikali ya Israel”, chuo hicho kimekumbusha kuwa takribani mwaka mmoja umepita tangu azimio jingine kama hilo lililopitishwa Septemba 2024. Mara hii, Unicamp imerudia kulaani vurugu dhidi ya raia wa Kipalestina na kuitaka Serikali ya Brazil kuungana na taasisi nyingine za kimataifa na kitaifa kusitisha mahusiano ya kibiashara na kijeshi na Israel.
Kundi la wanafunzi na wahadhiri “Unicamp em Movimento” limeeleza katika maandiko ya azimio hilo kuwa misimamo kama hii tayari imewahi kupitishwa kupitia mitandao ya ushirikiano wa vyuo vikuu vinavyounga mkono taifa la Palestina, na sasa Unicamp inapaswa kuungana na taasisi nyingine za elimu na vuguvugu za kijamii ndani na nje ya Brazil kudai kukomeshwa kwa mauaji ya kimbari na kuunga mkono haki ya Wapalestina ya kujiamulia mustakabali wao.
Hatua hii mpya ya Baraza la Chuo Kikuu cha Jimbo la Campinas inaonyesha mwendelezo na kuimarika kwa mwitikio wa vyuo vikuu kuhusu mgogoro wa kibinadamu Gaza. Kwa kuepuka lugha ya kidiplomasia ya kawaida, na kutumia misemo mikali kama “mauaji ya kimbari” pamoja na wito wa kusitisha mahusiano na Israel, Unicamp imechukua msimamo wa kipekee na wenye uzito mkubwa.
Your Comment