vikwazo
-
Tukio la “Iran Moyo Mmoja”:
Sheikh Naeem Qassem: Iran Daima Iko Kando ya Muqawama / Mmekuwa Mfano kwa Dunia Nzima
Sheikh Qassem pia aliipongeza Iran ya Kiislamu kwa kusimama kwake kwa ushujaa mkubwa dhidi ya uvamizi wa Marekani na Israel kwa kipindi cha siku kumi na mbili, akisema: “Alhamdulillah, mmeonyesha mfano kwa dunia nzima jinsi ya kupambana na uvamizi, kusimama imara, na kufikia mafanikio makubwa kwa baraka za uongozi wa Imam Khamenei (h.a), umoja wa watu na uaminifu wa wanajeshi wenu shupavu. Ushindi huu utaandikwa katika historia.” Akaongeza kwa kusisitiza: “Tunajua Iran inalipa gharama kubwa kwa kusimama upande wa haki, upande wa muqawama, upande wa Palestina, na upande wa mataifa yote yanayohitaji msaada. Lakini hii ndiyo Iran — mfano wa kujitolea, utukufu na uadilifu — ambayo haidai chochote kwa kusimama na wanyonge. Iran hii imesimama kwa ajili ya utukufu wa ubinadamu.” Sheikh Qassem alizungumzia pia vikwazo vipya dhidi ya Iran, akisema: “Leo tena wameiwekea Iran vikwazo vipya. Je, vikwazo hivi viliwahi kuacha kuwepo? Tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu miaka 46 iliyopita, Iran imeendelea kuwa chini ya vikwazo, lakini kila siku taifa hili limeendelea kung’aa zaidi na kuthibitisha kuwa ni taifa la ukweli na la mapambano.”
-
Abu Muhammad al-Jolani Kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Huku Akiwa Chini ya Vikwazo
Ahmad al-Sharaa, maarufu kama Abu Muhammad al-Jolani, Rais wa Serikali ya Muda ya Syria, anatarajiwa kushiriki na kutoa hotuba katika kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York katika wiki chache zijazo.
-
Waumini wa Kabul Waadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (a.s) Wakihoji Vikwazo vya Safari za Mahujaji (Mazuwwari) wa Afghanistan
Sambamba na kuwadia kwa siku ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s), hafla ya kuadhimisha siku hii ilifanyika katika Kituo cha Fiqhi cha Maasemamu Watakatifu (a.s) upande wa magharibi mwa jiji la Kabul. Washiriki, sambamba na kufanya maombolezo kwa ajili ya Imam Hussein (a.s), walitoa malalamiko makali dhidi ya ukosefu wa uratibu wa kisiasa na kisheria ambao mwaka huu uliwazuia waumini wengi wa Afghanistan kusafiri kwa wingi kwenda Karbala.
-
Vikwazo vya kuibuka kwa “tofauti za kitabaka” kama chanzo cha kuporomoka kwa jamii katika Uislamu
Uislamu, ili kuzuia kuporomoka kwa jamii kunakosababishwa na tofauti za kitabaka, umezingatia misingi ya kimaadili na kiitikadi kama vile tauhidi na uadilifu, na kwa kuweka hukumu za kiuchumi kama vile zaka, khumsi na kuharamisha riba, pamoja na kubainisha majukumu ya serikali ya Kiislamu, unalenga kusambaza mali kwa uadilifu na kusaidia wahitaji. Hatua hizi zimekusudiwa kuunda jamii yenye usawa na iliyo mbali na ufa mkubwa wa kitabaka.
-
A'shura ni ishara ya uvumilivu katika vyombo vya habari vya Bahrain, lakini kwa kweli, ni eneo la ukandamizaji dhidi ya Mashia
Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Bahrain amesema: A'"shura inatolewa kila mwaka katika vyombo vya habari vya Bahrain kama ishara ya uhuru na uvumilivu wa kidini, lakini kivitendo wafuasi wa Kishia wanakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria na vikwazo vikali, kuanzia kukamatwa na kuandikiwa wito hadi kuharibiwa maeneo ya kidini na mashinikizo ya kubadili mavazi ya kidini.
-
Iran imeapa kutoa jibu "kali" ikiwa itawekewa tena vikwazo vya Magharibi kupitia Umoja wa Mataifa
Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) Behrouz Kamalvandi anasema kuhusu nchi za Magharibi: Iran imezionya nchi za Magharibi dhidi ya kichochezi cha "kidhalimu" cha "kuwekea kwa mara nyingine tena" vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu katika Umoja wa Mataifa, akisema kwamba Iran itatoa jibu kali la kutisha.