25 Januari 2020 - 15:15
Sheikh Akramah azuiliwa tena kuingia Masjidul Aqsa

Polisi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mara nyingine tena wamempiga marufuku Sheikh na mhadhiri wa msikiti wa Masjidul Aqsa Sheikh Akramah Sabri kuingia na kuhutubia katika msikiti huo

Shirika la habari la Ahlubayt (as):

Polisi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mara nyingine tena wamempiga marufuku Sheikh na mhadhiri wa msikiti wa Masjidul Aqsa Sheikh Akramah Sabri kuingia na kuhutubia katika msikiti huo kwa muda wa miezi minne.

Hatua hiyo inakuja baada ya Polisi hao leo asubuhi kuingia nyumbani kwa Shekh Akramah na kumtaka siku ya kesho (Jumapili) aripoti kituoni kwa ajili ya mahojiano kamili.

Si mara ya kwanza kwa muhadhiri huyu wa msikiti huu kuzuiliwa kuingia msikitini hapo, ikumbukwe mwaka 2004 aliwahi kuzuiliwa kwa muda wa miezi minne, na hata hivi karibuni alizuiliwa kwa muda wa wiki moja.