Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Rouhani ameyasema hayo leo mjini Tehran wakati wa kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Corona ambapo ametangaza hatua kadhaa zitakazochukuliwa kukabiliana na janga la corona. Rais Rouhani amesema watakaokuwa na jukumu la kutekeleza sheria ya kuhakikisha wote wanavaa barakoa ni Jeshi la Polisi na Jeshi la Kujitolea la Wananchi (Basiji). Aidha kila atakayekiuka sheria ya kukaa katika karantini atatozwa faini ya riali milioni mbili.
Rais Rouhani amesema sheria hiyo ya barakao na karantini inahusiana na mji wa Tehran kwa sasa na kuongeza kuwa iwapo, itahitajika sheria hiyo inaweza pia kutumiwa katika miji mingine ya Iran. Hali kadhalika amesema Iran imetanga dola milioni 100 kununua vifaa vya kupima corona kutoka nchi za kigeni na kwa msingi huo kutakuwa na mabadiliko makubwa katika vipimo hivyo hivi karibuni.
Rais wa Iran ameashiria wimbi jipya la maambukizi ya corona duniani na kusema hali hii imejitokeza kutokana na upuuzaji wa misingi ya kiafya.
342/