Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya India Express, Maulana Mahmoud Asad Madani, mkuu wa Jumuiya ya Maulamaa wa India amesema, Waislamu katika wilaya ya Sultanpur kwenye jimbo la Uttar Pradesh walishambuliwa na kujeruhiwa na Wahindu baada ya kuwataka Wahindu hao wapunguze sauti ya muziki wakati wao Waislamu walipokuwa wanasali.Shambulio na hujuma hiyo ya Wahindu ilisababisha pia hasara na uharibifu kwa msikiti wa Waislamu, na Wahindu hao wakashambulia pia maduka kadhaa ya Waislamu na skuli moja katika eneo la Ibrahimpur na kusababisha hasara na uharibifu katika skuli hiyo.Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi imewawekea vikwazo na vizuizi vingi Waislamu wa nchi hiyo. Siasa na sera za serikali ya India za kukandamiza na kukiuka haki za Waislamu zimepelekea Wahindu wenye itikadi na misimamo mikali, wanaoungwa mkono na chama tawala cha BJP chenye misimamo ya kufurutu mpaka ya utaifa wa kihindu, kuchukua hatua mbalimbali za kuwashambulia na hata kuwaua Waislamu wa nchi hiyo.../
16 Oktoba 2022 - 16:23
Msimbo wa Habari: 1314303
Jumuiya ya maulamaa wa Kiislamu wa India imewataka viongozi wa nchi hiyo katika jimbo la Utta Pradesh wakomeshe kile ilichokiita "hatua ya upande mmoja" dhidi ya Waislamu.