Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametangaza vifo hivyo leo jioni baada ya kuwasili kwenye eneo ilipotokea ajali hiyo.
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi kutokana na ndege hiyo kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Mkoa wa Kagera na kutumbukia Ziwa Victoria ambalo lipo karibu na uwanja huo.
Ndege hiyo ilikuwa na watu 43, kati yao 39 wakiwa abiria, marubani wawili na wahudumu wawili ambapo tayari 28 wameokolewa.
Kwa mujibu wa taarifa ndege ya Precision Air namba PW494 ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kupitia Bukoba,
ilianguka katika Ziwa Victoria leo asubuhi, muda mfupi kabla ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amesema watu 19 wamethibitishwa kufariki dunia na kuna watu 26 waliojeruhiwa mbao ni manusura wa ajali hiyo.
Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha sehemu ya ndege hiyo iliyozama ikiwa imezungukwa na boti za uokoaji.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kutokana na mkasa huo.
Katika ujumbe wake, Rais Samia amesema: "Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya ndege ya Shirika la Precision katika Ziwa Victoria, mkoani Kagera. Natuma salamu za pole kwa wote walioathirika na ajali hii. Tuendelee kuwa watulivu wakati huu zoezi la uokoaji likiendelea huku tukimuomba Mwenyezi Mungu atusaidie."
342/