Sayyid Raisi alisema hayo jana kwenye kikao cha Baraza lake la Mawaziri na kusisitiza kuwa, adui amejeruhiwa na Mapinduzi ya Kiislamu na ndio maana amefanya njama kubwa ya kuanzisha vita vya kila upande na vya pande zote ili kujaribu kuzuia ustawi wa Iran kupitia kutoa pigo kwa usalama, uchumi, elimu, uzalishaji wa bidhaa na kujitegemea taifa la Iran. Lakini amesema, sambamba na jitihada zaidi za taasisi za serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi, taasisi za usalama kama polisi na vikosi vya ulinzi, nazo zinatekeleza majukumu yao makubwa na mazito ya kulinda usalama wa wananchi na wa rasilimali za taifa.
Vile vile amegusia uungaji mkono wa wazi wazi kabisa wa Marekani, Ufaransa na nchi kadhaa za Ulaya kwa vitendo vya kigaidi na machafuko ya hivi karibuni humu nchini na kuzionya nchi hizo akisema, bila ya shaka yoyote kuunga mkono ugaidi na machafuko si kwa manufaa yao hata kidogo.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vile vile amesema ni jambo linalotia huzuni na kuumiza sana jinai za wafanya fujo na magaidi za kuwaua shahidi kidhulma watoto wadogo, wanawake, wanaume na mafisa wa kulinda usalama wa Iran na kuongeza kuwa, hatua kali na za haraka zitaendelea kuchuliwa dhidi ya wote waliohusika na mauaji hayo.
342/