Watu kadhaa waliokuwa na silaha leo wametekeleza shambulio la kigaidi katika kituo cha polisi cha 16 huko Zahedan makao makuu ya mkoa wa Sistan na Baluchistan; ambapo makabiliano ya risasi yalijiri kwa masaa kadhaa na kupelekea kuuliwa shahidi maafisa wawili wa polisi na magaidi kadhaa kuangamizwa.
Taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imebainisha kuwa magaidi wote wanne waliokishambulia kituo cha polisi cha Zahedan wameuawa. Shambulio hilo lilianza baada ya watu waliokuwa na silaha huku wakitumia maguruneti walipojaribu kujipenyeza katika kituo hicho cha polisi.
Ali Reza Marhamati Naibu Gavana wa Mkoa wa Sistan na Baluchistan anayehusika na masuala ya usalama ameeleza kuwa shambulio hilo la kigaidi lilianza saa moja na robo leo asubuhi, ambapo askari usalama walifanikiwa kudhibiti hali ya mambo kwa kuwepo kwa wakati katika eneo la tukio. Amesema, magaidi walidhibitiwa kabla ya kuingia katika kituo cha polisi.
342/