YouTube imechukua hatua hiyo katika hali ambayo Wamagharibi wamejitambulisha kizandiki kuwa ni watetezi wakubwa kabisa wa uhuru wa kutoa maoni unaotajwa kama msingi mkuu wa demokrasia ya Uliberali.Ikumbukwe kuwa tangu vilipoanza vita vya kidhalimu vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza, mitandao ya kijamii ya Marekani na Magharibi, imekuwa ikitumia visingizio hewa na vya uongo vinavyogongana waziwazi na uhuru wa kutoa maoni ili kuzifuta au kuziwekea vizuizi na mipaka akaunti za watu binafsi, taasisi au makundi yanayoweka hadharani jinai za kinyama zinazofanywa na Israel huko Ghaza.Jumapili usiku, jeshi la utawala ghasibu wa Israel lilishambulia kwa makombora kambi ya wakimbizi katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza na kuwaua shahidi Wapalestina wasiopungua 45 wakiwemo wanawake na watoto na kujeruhi wengine 249.
342/