Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Kaburi la Hadhrat Ayoub (as) liko "Bayt Zarbij", Kilomita 27 Kaskazini-Magharibi mwa Mji wa Salalah nchini Oman, na linachukuliwa kuwa mojawapo ya vivutio muhimu vya Watalii katika eneo hilo.
Kuna chemchemi karibu na Kaburi la Hadhrat Ayoub iitwayo Chemchemi ya Shardat, na hadithi zinasema kwamba Chemchemi hiyo ilianza kutiririsha maji baada ya Hadhrat Ayoub (as) kumuomba Mola wake amuondolee balaa.
Jina la Ayoub limetajwa mara 4 katika Surah za: Al-Nisaa, Al-An'am, Al-Anbiyaa, na Raad.
Nabii huyu alijulikana kwa uvumilivu wake, kiasi kwamba mpaka uvumilivu wame ukawa methali (na mfano hai); na alipoteza watoto wake mmoja baada ya mwingine na akaugua.
Katika Uislamu, Hadithi yake (kisa chake) inadhihirika (na kuchukuliwa) kama moja ya mifano hai ya Mwenyezi Mungu katika kuwalipa ujira wenye subira; na kuzingatiwa kwa subira kuwa ni yenye thamani kubwa na muhimu katika Dini hii Tukufu ya Kiislamu.
Inasemekana kwamba nchi ya asili ya Hadhrat Ayoub (a.s) ni ardhi ya Aus. Ingawa bado hakuna kitu ambacho kimethibitishwa kuhusu mahali alipoishi, wengine wanaamini kwamba aliishi "Sham" au panapojulikana leo hii kama Syria Kubwa.
Saeed Al-Hashli, Afisa wa Wizara ya Habari ya Oman, anasema:
"Ukumbi huu wa Sala ni sehemu ya Madhabahu -Haram- ya Hadhrat Ayoub (a.s), kama unavyoona, kuna vibla viwili kwa ajili ya kuswali. Kibla hiki kinaelekea Jerusalem (Quds). Baada ya kubadilisha uelekeo wa Kibla kutoka Beit al-Maqdis hadi Makka, Kibla (mwelekeo wa) cha Sala kikabadilika na kuwa katika upande huu.
Kaburi la Hadhrat Ayoub (as) lina Upana wa Mita 4 na Urefu wa Mita 1.5; na ni moja ya sehemu zinazotembelewa sana na Watalii huko Salalah.