2 Oktoba 2024 - 20:03
Spika wa Bunge: Tumewaonyesha wavamizi sehemu ndogo tu ya uwezo wa Iran

Mohammad Baqir Qalibaf, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza operesheni ya makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH dhidi ya utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa, wavamizi wameonyeshwa sehemu ndogo tu nguvu ya Iran.

Spika Qalibaf ameandika ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba: Kwa nguvu zetu zote na kwa kuzingatia haki halali ya kujihami, tunasimama dhidi ya uchochezi wa kivita utawala wa Kizayuni. Kuliandaliwa majibu ambayo hayakutarajiwa kabisa dhidi ya vitisho vya adui, majibu yasiyotarajiwa yameundwa.  Laiti mngejua kilichotayarishwa kwa ajili yenu, mngeacha sasa kuitisha Iran.

Spika wa Bunge la Iran amesisitiza kuwa, Operesheni Ahadi ya Kweli -2 iliyotekelezwa jana na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH limeufedhehesha utawala haramu wa Israel kijeshi na kipropaganda.

"Katika Operesheni Ahadi ya Kweli -2, vituo kadhaa vya anga na rada, pamoja na vituo vya njama na mipango ya mauaji dhidi ya viongozi wa Muqawama na makamanda wa IRGC vimelengwa", imesema taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

IRGC imesema kuwa ingawa maeneo yaliyopigwa yamelindwa na mifumo ya hali ya juu ya ulinzi, lakini 90% ya makombora ya balestiki ya Iran yamepiga kwa mafanikio shabaha zilizokuisudiwa.

"Utawala wa Kizayuni umepatwa na wahka kutokana na uwezo wa kiintelijensia wa kioperesheni wa Jamhuri ya Kiislamu," imeongeza taarifa ya IRGC.

342/