Maafisa wa serikali ya Sweden walitangaza kwamba wamechoma moto maiti ya Salwan Momika, aliyevunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini humo, baada ya kukosekana mtu yeyote wa kupokea maiti hiyo.
Kwa mujibu wa chapisho la Current Report, viongozi wa Sweden waliwasiliana na jamaa zake mara kadhaa lakini hawakupata jibu.
Momika, ambaye alijiarifisha kuwa mwanaharakati wa kupinga Uislamu, alipigwa risasi na kuuawa Januari 29 alipokuwa akitoa ujumbe moja kwa moja kwenye TikTok katika eneo la Hovsjo nchini Sweden.
Maafisa wa Sweden hawakutoa maelezo kuhusu majivu ya maiti yake yalipotumwa au hatua zozote za kisheria zinazohusiana na kesi yake.
Momika, ambaye alipata umaarufu duniani kwa vitendo vyake vya vya kuchoma moto nakala ya Qur'ani mbele ya balozo za nchi kadhaa za Kiislamu, hivi karibuni alikimbilia Norway baada ya kutimuliwa Sweden.
Mnamo Juni 2023, Salwan Momika alikanyaga Qur'ani kabla ya kuteketeza moto kurasa zake kadhaa mbele ya msikiti mkubwa zaidi wa Stockholm. Kitendo hicho kiovu cha kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu kilifanywa chini ya idhini na ulinzi wa polisi wa Uswidi.
Tukio hilo lililosadifiana na siku kuu ya Idul al-Adha liliibua hasira za Waislamu kutoka sehemu mbalimbali duniani.
342/
