Wachambuzi wa masuala ya nishati wanasema Marekani imezalisha umeme mwingi zaidi wa nyuklia kuliko nchi nyingine yoyote, na tangu 1990 mitambo yake imesambaza karibu asilimia 20 ya jumla ya nishati ya umeme nchini humo kwa mwaka, kiwango ambacho kinatosha kudhamini umeme wa zaidi ya nyumba milioni 70. Utawala wa Biden pia uliitambua nishati ya nyuklia kuwa njia ya kukidhi mahitaji katika uwanja huo bila uzalishaji wa gesi chafu, na serikali yake uliweka lengo la angalau kuzidisha mara tatu nishati ya nyuklia nchini Marekani ifikapo 2050.
Sisitizo la serikali ya Trump la kuzidisha matumizi ya nishati ya nyuklia na kutilia mkazo udharura wa kustawishwa zaidi vinu vipya vya nyuklia nchini Marekani linakuja wakati Washington ina mtazamo tofauti kabisa kuhusiana na utumiaji wa teknolojia ya amani ya nyuklia na nishati ya nyuklia katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Donald Trump na maafisa wa ngazi za juu wa utawala wake, bega kwa bega na utawala wa Kizayuni wa Israel, daima wamekuwa wakitaka kusitishwa shughuli za kuzalisha nishati ya nyuklia na kufungwa vituo vya nyuklia vya Iran, wakidai kuwa Jamhuri ya Kiislamu inataka kupata silaha za nyuklia, bila ya kutoa ushahidi wowote kuhusu suala hili.
Marekani inatumia hata vitisho dhidi ya Iran ili kufikia lengo hilo, na inasisitiza kuwa, machaguo yote yako mezani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Haya yanajiri licha ya kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikisema mara kwa mara kwamba, sio tu haina mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia, bali hata haina mwelekeo huo.
Kinyume na tuhuma zisizo na msingi za Washington na Tel Aviv kwamba Tehran ina nia ya kupata silaha za nyuklia, Iran imeweza kutumia teknolojia ya nyuklia ya amani kwa kiasi kikubwa katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kuzalisha umeme, dawa, kilimo na maeneo mengine.
Inaonekana kwamba, suala la kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kujenga vinu vipya vya nishati ya nyuklia limepewa mazingatio makubwa kwa kuzingatia dira ya mahitaji ya umeme ya Iran.
342/
