8 Machi 2025 - 17:40
Source: Parstoday
Nini kinaendelea Syria? Taasisi za kimataifa kimya!

Ukimya wa taasisi za kimataifa kuhusiana na mauaji ya umati dhidi ya raia nchini Syria yanayofanywa na viongozi wenye mafungamano na utawala wa al-Julani kwa mara nyingine tena unathibitisha undumilakuwili wa taasisi hizo.

 wakati watu wenye mfungamano na serikali ya al-Julani wakifanya mauaji makubwa ya raia nchini Syria jana usiku, taasisi za kimataifa, hususan Baraza la Usalama, hazijaguswa na mauaji hayo ya kutisha.

Abu Mohammad al-Julani, mkuu wa serikali ya mpito nchini Syria, alisema jana usiku kuhusuu maandamano ya wananchi wa Syria wa mikoa ya kaskazini mwa nchi hiyo kwamba: "Hatutoruhusu kuchafuliwa amani ya ndani ya nchi." Alidai kuwa vikosi vinavyoshirikiana na utawala wa Bashar al-Assad vinapanga kuitumbukiza Syria katika machafuko.

Al-Julani ametoa madai hayo wakati Mazloum Abdi, kamanda wa kabila la Kikurdi wa Syrian Democratic Forces (SDF), amepinga madai hayo ya al-Julani ni kusisitiza kuwa, hakuna hata mwanajeshi mmoja mwenye uhusiano na utawala wa Bashar al-Assad aliyeko katika mikoa ya kaskazini na mashariki mwa Syria.

Mtandao wa televisheni ya Al-Mayadeen nao umenukuu taarifa ya Shirika la Haki za Binadamu la Syria na kutangaza kwamba, kumefanyika mauaji makubwa matano tofauti katika maeneo ya pwani ya Syria, ambapo raia 162, wakiwemo wanawake na watoto wadogo wameuawa.

Kuhusiana na hilo, Baraza la Kiislamu la Alawite nchini Syria limetoa taarifa na kutahadharisha kuhusu kupanuka migogoro na mauaji ya raia nchini humo. Lakini Baraza la Usalama na taasisi za kimataifa zimenyamaza kimya mbele ya mauaji ya raia nchini Syria.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha