Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (AS) - Abna - Kituo cha Jumuiya ya Utamaduni wa Iran kimeundwa nchini Ghana, sambamba na kuunda mtandao wa kimawasiliano miongoni mwa Wahitimu wa Ghana wa Vyuo Vikuu vya Iran na kutumia uwezo wa ndani katika njia ya kuendeleza uhusiano wa kitamaduni kati ya Tehran na Accra.
Katika kikao cha kwanza cha Jumuiya hii, Amir Heshmati, mshauri wa kiutamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ghana, akigusia nafasi ya asasi za ndani na zisizo za Kiserikali katika kuendeleza uhusiano wa kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili, aliwachukulia wahitimu wa Ghana wa Vyuo Vikuu vya Iran kuwa ni uwezo usioweza kubadilishwa kwa ajili ya kuendeleza uhusiano wa kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili.
Kwa kutambulisha mifano ya mafanikio ya (jumuiya au) vyama vya kitamaduni, alisema kuwa kutumia uzoefu wa (jumuiya au) vyama vya kitamaduni ni njia ya uhakika ya kuharakisha shughuli (harakati).
Mshauri wa masuala ya kiutamaduni wa Iran nchini Ghana ametaja kutambuliwa ladha, maslahi na mahitaji ya jamii inayolengwa kuwa ni sharti muhimu la ufanisi wa mipango ya Jumuiya ya Utamaduni ya Iran nchini Ghana na kusema: Mshauri wa Utamaduni yuko tayari kuunga mkono Jumuiya hii katika kustawisha uhusiano wa kiutamaduni kati ya nchi hizi mbili.
Katika muendelezo wa mkutano huu, kila mmoja wa wanachama wakuu wa Jumuiya hiyo, wakati akitoa maoni yake, alitangaza kuundwa na kuanzishwa kwa Jumuiya ya Utamaduni ya Iran nchini Ghana kuwa ni fursa ya kujumuika pamoja na ushirikiano wa wahitimu wa Ghana wa Vyuo Vikuu vya Iran.
Mwishowe iliamuliwa; Kuanzia Mwezi Aprili mwaka huu (2025), ili kubuni na kutekeleza programu, mikutano ya kila wiki ya jumuiya hii, inapaswa kuwa ikifanyika katika mahali pa mashauriano (katika Kituo cha Utamaduni cha Iran).
Your Comment